TRA YAKANUSHA KUFUNGWA BANDARI YA BAGAMOYO, YATANGAZA UJIO WA UTARATIBU MPYA
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Pwani inakuja na utaratibu mpya kwa wafanyabiashara wa mafuta katika Bandari ya Bagamoyo wanaosafirisha bidhaa hiyo kutoka Zanzibar, hatua itakayoanza kutekelezwa kuanzia Machi, 2026 kwa lengo la kuboresha ukusanyaji kodi ulio rafiki kwa wafanyabiashara hao.
Aidha, mamlaka hiyo imekanusha taarifa za kufungwa kwa bandari hiyo na kuwataka wachukuzi, wafanyabiashara na wananchi kupuuza propaganda zinazosambazwa.
Akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu huo katika mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta, wajasiriamali na wachukuzi uliofanyika Februari 27, 2026, Meneja wa TRA Pwani, Masawe Masawe, amesema kwa niaba ya Kamishna Mkuu kuwa lengo la serikali ni kujenga mazingira rafiki ya biashara sambamba na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga ameeleza kuwa bandari hiyo ni kitovu muhimu cha ajira ambapo takribani vijana 400 wanategemea shughuli mbalimbali za kiuchumi, na kusimama kwa biashara hiyo kuliathiri kipato na zoezi la usajili wafanyabiashara.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Shaban Hamsini, ameelezea kuzorota na kusuasua kwa shughuli bandarini kuliathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa wafanyabiashara na mapato ya halmashauri .
Diwani wa Kata ya Dunda, Amir Mpwimbwi, ameishukuru serikali kwa kushughulikia changamoto hiyo na kueleza matumaini kuwa uchumi wa eneo hilo utarejea katika hali yake ya kawaida .
Mchukuzi wa madumu ya mafuta, Wema Abdallah, amesema wamechoka kukaa bila kazi kwa zaidi ya miezi miwili, hali iliyowakosesha kipato cha kujikimu.
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment