MIRADI 68 PWANI YAPITISHWA, MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA HAKUNA DOSARI
MWENGE wa Uhuru umeridhishwa na utekelezaji wa miradi yote 68 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 263.1 mkoani Pwani, ukibainisha kuwa hakuna mradi wenye dosari.
Mwenge huo umepitia wilaya saba zenye halmashauri tisa katika mkoa huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang’onda, amepongeza mkoa wa Pwani kwa usimamizi mzuri wa miradi, akieleza kuwa wananchi wengi, wakiwemo wazee, wamefanikiwa kuuona Mwenge wa Uhuru katika maeneo ya ndani kwa mara ya kwanza, huku wengine wakidai hawajauona kwa miaka mingi.
Amesema mikoa na halmashauri nyingine zinapaswa kuiga mfano wa Pwani kwa kuhakikisha miradi inaelekezwa katika maeneo yatakayowezesha Mwenge kufika kwa wananchi wengi zaidi.
Kwa mujibu wa Mwang’onda wamefika Ndundutawa, Kata ya Shela, Rufiji wananchi hawajawahi kuuona Mwenge kwa miaka mingi.
Ameomba mikoa na halmashauri nyingine ziige mfano huu ili wananchi waweze kuushuhudia Mwenge wao.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kulinda na kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa, wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa mkoa wa Lindi katika eneo la Somanga Aprili 27, 2026.
Amefafanua kuwa kati ya miradi hiyo, miradi 23 imewekewa mawe ya msingi, 17 imezinduliwa na 24 imekaguliwa.
Mwenge wa Uhuru 2026 unabeba ujumbe wa kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa chini ya kaulimbiu isemayo: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo.”
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Post a Comment