TUME YA UCHUNGUZI MATUKIO YA UVUNJIFU WA AMANI YAKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 17, 2026.
Mkutano huo ambao umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzanja (BOT) jijini hapa, ni sehemu ya juhudi za Tume hiyo kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali.
Pamoja na mambo mengine, hoja zilizojadiliwa katika mkutano huo zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa na kimataifa.
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo waathirika wa matukio ya uvunjifu wa amani, kwa lengo la kukusanya ushahidi na taarifa zitakazoiwezesha kuandaa ripoti ya kina.

Post a Comment