BILA TUMBO LA TEMBO SI MBEGU YA UBUYU WALA UKWAJU ITAOTA

Mimea yenye mbegu ngumu kama ukwaju na ubuyu haiwezi kuota ardhini bila kupita katika mfumo wa mmeng'enyo wa tumbo la tembo lenye utumbo wa mita 14 na kufanya ganda lake kulainika na kuanguka ardhini kama kinyesi hali ambayo huifanya mbegu hiyo kuota

Haya yamebainishwa na Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI) bwana Revocutus Meney anayeshughulika na Utatuzi wa Changamoto ya wanyama wakali na waharibifu kupitia mazao mbadala wakati akitoa mada kwenye Kongamano la maadhimisho ya Siku wa Wanyamapori duniani ambayo Kilele chake kitakuwa tarehe 3 Machi, 2026.

Aidha Bwana Revocatus aliongeza kuwa Mnyama Tembo kabla ya Kupata uhuru kulikuwa na tembo wanaofikiwa 300,000 ila kwa sasa kuna tembo Takriban 61,000 pamoja na kwamba tembo wanaonekana kupungua lakini kumekuwa na changamoto kubwa ya Binadamu kuingia kwenye maeneo ambayo tembo wamekuwa wakitumia kama makazi yao.

Katika hatua nyingine Mtoa maada kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka Dkt. Never Mwambela alisema kuwa Mimea dawa si uchawi ni sayansi ya mimea ni dawa asili za mimea ni muhimu sana hutibu magonjwa mbalimbali na katika kukuza uchumi kwani kadri tunavyo kwenda tunazidi kutumia mimea dawa, alipokuwa akitoa mada ya Matumizi na biashara ya mimea dawa na manukato tanzania

Kongamano hilo ni moja ya shughuli zinazofanyika katika viwanja vya Nanenane kuadhimisha siku ya wanyamapori Duniani ambapo mada zingine zilizowasilishwa ni Utekelezaji wa mkataba wa cities kwa nchi ya Tanzania na Fursa za matumizi ya mimea dawa katika kutibu magonjwa ya binadamu hapa Tanzania.

No comments