DKT. IDRIS RASHID AFARIKI DUNIA, RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE
Aliyekuwa Gavana wa Nne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Idris Rashid, amefariki dunia ambapo taarifa za awali za kifo chake zimetoka usiku huu.
Kufuatia kifo hicho,Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole akieleza kuwa amepokea kwa huzuni taarifa za kifo cha kiongozi huyo aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.
Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa Dkt. Rashid atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, hasa katika kuimarisha sekta za fedha na nishati nchini.
Rais Samia pia ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na wote walioguswa na msiba huo, akisisitiza kuwa taifa limepoteza mchumi mbobezi na kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na ushauri kwa taasisi za umma na sekta binafsi.

Post a Comment