LEO NI SIKU YA HISABATI DUNIANI, TUAMBIE UNAVUTIWA NA NINI KATIKA SOMO HILI


Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha SIKU YA HISABATI DUNIANI, ambapo wadau wa elimu, wanafunzi na wataalamu wa sayansi wanahimizwa kutambua mchango wa hisabati katika maendeleo ya jamii. 


Maadhimisho hayo yanaratibiwa kimataifa na UNESCO kwa kushirikiana na International Mathematical Union pamoja na IMAGINARY, kupitia kongamano la kimataifa la mtandaoni lenye kaulimbiu ya “Hisabati na Matumaini”.


Siku hiyo ilitangazwa rasmi mwaka 2019 na tangu wakati huo imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa hisabati katika sayansi, teknolojia na maendeleo ya jamii.

 

Kwa Tanzania, wadau wa elimu wanaeleza kuwa taaluma ya hisabati ni muhimu katika kuwajengea vijana uwezo wa kufikiri kwa kina na kushiriki katika uchumi wa kisasa unaotegemea maarifa na teknolojia.

No comments