DKT. MUYUNGI ASISITIZA KASI UJENZI WA JENGO LA OMR- MTUMBA DODOMA


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dokta Richard Muyungi amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Suma JKT kuongeza kasi ya ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Dokta Muyungi amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo ambapo aliongozana na Viongozi na Menejimenti kwa ajili ya kujionea na hatua iliyofikiwa katika mradi huo.

Amesema mkandarasi wa kampuni ya Suma JKT hana budi kufanya kazi masaa 24 ili kuwezesha maboresho na ukarabati wa baadhi ya maeneo ndani ya jengo ambayo hayajakamilika.  

Dokta Muyungi amesema Ofisi yake haitongeza muda wa kukamilisha mradi huo kwa kuwa ilishafanya hivyo hapo awali na hivyo kumtaka mkandarasi hukakikisha anatumia vyema muda uliopo kuweza kukamilisha na kukabidhi jengo hilo.



No comments