TPSF YAPOKEA UGENI WA GROUP CEO WA ABF SUGAR AMBAO NI WAMILIKI WA KILOMBERO SUGAR


Rais wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula, akishirikiana na Mwakilishi wa Kongani ya Kilimo wa TPSF, Bw. Jitu Son, walimpokea Bw. Paul Kenward, Group CEO wa ABF Sugar, kampuni mama na mmiliki wa Kilombero Sugar katika kikao maalum kilicholenga kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi na wawekezaji wakubwa nchini

Katika kikao hicho pia alikuwepo CEO wa Kilombero Sugar Bw. Guy Williams ambaye alimsindikiza Bw. Paul Kenward katika ziara hiyo. Mazungumzo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya TPSF na wawekezaji wakubwa wa kimataifa, pamoja na kujadili namna sekta binafsi inavyoweza kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania

Kupitia uwekezaji wake nchini, Kilombero Sugar imeendelea kuwa miongoni mwa wawekezaji wakubwa katika sekta ya kilimo, ikichangia ajira za moja kwa moja zaidi ya 5,000 na kuwahusisha takribani wakulima wadogo 10,000 wa miwa wanaonufaika moja kwa moja na shughuli zake. Uwekezaji huu umeendelea kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii zinazozunguka maeneo ya uzalishaji.

Aidha, Bw. Paul Kenward alisisitiza dhamira ya ABF Sugar kuendelea kuwekeza nchini na kuitangaza Tanzania kimataifa kama eneo lenye mazingira rafiki ya biashara na fursa nyingi za uwekezaji


No comments