KIHONGOSI AFIKISHA UJUMBE WA RAIS DKT SAMIA MKOANI KAGERA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu. 𝗞𝗲𝗻𝗮𝗻𝗶 𝗞𝗶𝗵𝗼𝗻𝗴𝗼𝘀𝗶 amewasili Mkoani Kagera na kupokelewa na wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi waliofika kwa ajili ya mapokezi yaliyofanyika mkoani humo, leo tarehe 26 Machi 2026.

Akizungumza baada ya kuwasili mkoani humo, Kihongosi amewasilisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, kwa wanachama na viongozi wa CCM Mkoa wa Kagera na kuwataka kuendelea kushikamana katika kufanya maendeleo ya miradi ya Serikali inayotekelezwa na chama hicho.

Kihongosi amesema kuwa ziara yake mkoani Kagera ni sehemu ya kuimarisha chama na kuhamasisha wanachama kujitolea kwa mujibu wa Ilani ya Chama ya 2025-2030.

Aidha, amewataka wanachama wa CCM kuendelea kuwa imara na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

No comments