MAREHEMU LUKUVI NI KIONGOZI MWENYE KUFANYA MAAMUZI KWA AJILI TA TAIFA - RAIS DOKTA SAMIA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amesema katika kipindi hiki ambacho Dunia inashuhudia misuguano na machafuko katika maeneo mbalimbali ambayo yanapelekea kupanda kwa gharama za maisha ikiwemo bei za bidhaa na mafuta, Taifa la Tanzania lilimuhitaji Waziri William Lukuvi kutokana na uzoefu wake wa Kiungozi ili ushauri wake uweze kulivusha Taifa.
Rais Samia amyasema hayo wakati wa kuaga mwili wa Marehemu William Lukuvi, katika viwanja vya Karimjee Posta Jijini Dar es salaam leo tarehe 28 Machi,2026.
Akizungumza na mamia ya waombolezaji waliojitokeza kutoa heshima ya mwisho, Rais Samia ameyasema haya;
“Lukuvi alikuwa Kiongozi aliyegusa mioyo ya Watu ambaye daima hakusita kusema ukweli na kuchukua maamuzi yenye tija na maslahi kwa Taifa, Ndugu zangu katika kipindi hiki ambacho Dunia imejaa mvuragano na machafuko tulihitaji Viongozi wenye uzoefu wa muda mrefu na waliofanya kazi maeneo mbalimbali Serikalini na kwenye siasa ili tuendelee na mawazo na ushauri, tulimuhitaji Lukuvi sasa kuliko jana lakini Mungu alimpenda zaidi”
Aidha, Rais Samia amezungumzia hali ya mchafuko wa kidunia inayoendelea sasa ya uwepo wa vita kwa baadhi ya mataifa ambapo amebainisha kuwa;
“Katika kipindi hiki dunia yetu imejaa msuguano ambayo kwa vyovyote vile yatapandisha hali ya maisha kuwa ngumu sio kwa Tanzania tu bali kwa Dunia, tumeanza kushuhudia upandaji wa bei za mafuta na tutashuhudia upandaji wa bei za bidhaa na kama vita hii itendelea tunategemea kuwa na mdororo wa uchumi Duniani, mambo ambayo yanataka umakini katika kufanya maamuzi katika Uongozi wa Nchi yetu, tumuombe Mungu haya yamalizike ili twende vizuri”
“Kwa uzoefu alionao Lukuvi tulimuhitaji sasa kuliko wakati wowote, kwasababu tunamkumbuka kwa moyo wa upendo pamoja na utayari wa kushirikiana na Watu katika maeneo mbalimbali, huu ndio urithi aliotuachia Mpendwa wetu Mhe. Lukuvi”
Post a Comment