NCHI WANACHAMA UMOJA WA MATAIFA WAKUTANA KUJADILI HALI YA WANAWAKE DUNIANI.
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekutana Jijini New York nchini Marekani kwa lengo la kujadili hali ya Wanawake katika nchi hizo.
Mkutano huo ni wa 70 kuhusu Hali ya Wanawake Duniani unaoongozwa na Kaulimbiu isemayo Kuhakikisha na Kuimarisha upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Wasichana wote, ikiwa ni pamoja na kukuza mifumo ya kisheria nyenye usawa na jumuishi, kuondoa sheria, sera, na desturi za kibaguzi na kushughulikia vikwazo vya kimuundo.
Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jana na utamalizika Machi 19 mwaka huu.
Mkutano utajadili masuala mbalimbali ya upatikanaji wa haki na huduma kwa Wanawake ikiwemo haki ya upatikanaji wa Ardhi, haki kwa upatikanaji wa Elimu, haki ya kujua masuala ya sheria na upatikanaji wa haki za kisheria, kushiriki katika masuala ya uongozi na siasa, haki ya kumilili na upatikanaji wa huduma bora za Afya.
Tanzania imeongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu, Wataalamu kutoka Wizara hiyo, Wizara nyingine za Kisekta, Taasisi za Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

.jpeg)
Post a Comment