RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA JAMHURI YA KIDEMOCRASIA YA CONGO AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA


Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (FECOFOOT), Jean-Guy Blaise Mayolas, amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa utakatishaji pesa, utengenezaji wa nyaraka za uwongo, pamoja na ubadhirifu wa pesa za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya soka la wanawake na ujenzi wa vituo vya michezo.


Uchunguzi ulibaini kuwa Mayolas alitumia karibu dola milioni 1.3 za fedha za FIFA kwa manufaa yake binafsi, na kutumia mtandao wa miamala ya kifedha ya bandia na rekodi za uwongo kuficha ukweli huo.


Sambamba na hilo Mke na mtoto wa Mayolas wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na makosa hayo huku Katibu Mkuu wa FECOFOOT, Badji Mombo Wantete, na Mhasibu, Raoul Kanda, wakihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja.


No comments