VITONGOJI UKANDA WA NYASA VYAFIKIWA NA MIRADI YA REA
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), umeendelea kutekeleza miradi ya kupeleka huduma ya umeme katika maeneo ya vitongoji ili kuwawezesha wananchi waliopo maeneo hayo kupata huduma bora ya nishati ya umeme kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa miradi ya REA, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Danstan Kalugira wakati akizungumza na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuhusu miradi inayotekelezwa na REA katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.
Kalugira amesema kiasi cha fedha takribani shilingi bilioni 3.1 tayari zimetolewa na Serikali kupitia REA ili kutekeleza mradi huo wa kupeleka umeme kwenye vitongoji takribani 6 vya wilaya ya Ludewa ili wananchi wanufaike na huduma ya umeme.
Amesema japokuwa kipindi hichi ni cha masika mvua nyingi zinanyesha ila mkandarasi huyo anaendelea kutekeleza mradi kwa kasi, weledi na ni matarajio kuwa atakwenda kumaliza mradi huo kwa wakati katika muda uliopangwa ili wananchi watakaounganishwa na nishati ya umeme waweze kunufaika.
Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha ya utekelezaji wa miradi hiyo inayoendelea katika mkoa wa Njombe na maeneo mengine nchini.
Ziara ya TEF imelenga kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na REA katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo miradi ya Awamu ya Pili B (HEP 2B) ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 9,009.
.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment