518 WAPOTEZA MAISHA KUFUATIA VURUGU BAADA YA UCHAGUZI, TUME YAKABIDHI RIPOTI NZIMA



Jumla ya watu 518 wamepoteza maisha kufuatia vurugu zilizotokea kabla na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio hayo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande.


Taarifa hiyo inaeleza kuwa mbali na vifo hivyo, watu 373 walifikishwa hospitalini wakiwa wamefariki dunia, huku wengine 121 wakijeruhiwa wakipatiwa matibabu katika vituo mbalimbali vya afya.


Jaji Chande amesema takwimu hizo zinaonesha uzito wa athari za vurugu hizo kwa jamii, akisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti ili kuzuia matukio kama hayo kujirudia katika chaguzi zijazo.


Aidha, amesema tume inaendelea kuchunguza kwa kina chanzo cha vurugu hizo pamoja na kuwabaini waliohusika, huku akitoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kushirikiana na mamlaka ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa nchini.








No comments