KISARAWE IKO TAYARI KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA KATIKA MACHO - MWANG'ONDA
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2026, Wazo Mwang'onda amekagua, kupokea taarifa na kuzindua huduma za kibingwa na upimaji macho Katika hospital ya Wilaya Kisarawe.
Mradi huo uliozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika hospital ya Wilaya Kisarawe Imegharimu zaidi ya Shilingi milioni 122.
Akiongea na wananchi, viongozi na wadau mbalimbali waliojitokeza katika Mbio za Mwenge Wilaya Kisarawe, Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Wazo Mwang'onda, amepongeza uwekezaji huo katika sekta ya Afya, upande wa Macho kwa kushusha huduma za kibingwa katika hospital ya Wilaya ili wananchi wapate huduma kwa ukaribu.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2026, Wazo Mwang'onda, amempongeza Rais wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha za Maendeleo katika miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Kuzinduliwa kwa Kitengo Cha Macho, na utoaji huduma za kibingwa katika hospital ya Wilaya ya Kisarawe, kunatoa taswira ya kutoa huduma za kibingwa kwa ukaribu za upasuaji na upimaji macho kwa wananchi.
Huduma zitazotolewa kuanzia jumatatu Hadi Ijumaa na Daktari Bingwa wa Macho Jackline Dominic.



Post a Comment