BWANKU ASHIRIKI SEMINA YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YA KUJENGEA UWEZO BODI ZA KUSULUHISHA MIGOGORO YA NDOA.
Jana Jumatano na leo Alhamisi, Wizara ya Katiba na Sheria inaendesha mafunzo kwa Bodi za Usuluhishi wa migogoro ya ndoa kwa mkoa wa Kagera yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kusuluhisha migogoro ya ndoa ili kujenga jamii yenye amani na maendeleo. Mafunzo yamefunguliwa Jana Jumatano na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Franklin Rwezimula.
Mafunzo yamehusisha Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ustawi, Wanasheria wa Halmashauri pamoja wa Wajumbe wa Bodi za Usuluhishi ngazi ya Kata.
Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku ameshiriki mafunzo hayo akimwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba ambapo watoa mada mbalimbali wametoa mafunzo akiwemo Mtaalamu wa Sheria za ndoa Prof. Cyriacus Binamungu kutoka Chuo Kikuu Mzumbe
Mada mbalimbali za mbinu za kusuluhisha migogoro ya ndoa zimetolewa lakini msisitizo umetolewa kwenye mafunzo hayo kwamba Bodi za Usuluhishi wa migogoro ya ndoa si sehemu ya kutoa hukumu bali kusuluhisha wanandoa na kuwa daraja la kuimarisha taasisi ya familia, ambayo ndio msingi wa jamii imara, ikiwa ni utekelezaji halisi wa dira ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kujenga taifa lenye mshikamano, maelewano na maendeleo endelevu.
Post a Comment