KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI IMEITAKA SERIKALI KUKAMILISHA MIRADI YA WIZARA NISHATI
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,imeishauri Serikali kuhakikisha inakamilisha na kupanga kwa ufanisi utekelezaji wa miradi yote iliyo chini ya Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake,ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokidhi ubora unaohitajika.
Akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo,leo April 27,2026 bungeni, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Simon Lusengekile, amesema usimamizi madhubuti wa miradi hiyo utawezesha utoaji wa huduma bora zaidi kwa wananchi, huku pia ukichochea ukuaji wa sekta ya madini kupitia miradi mikubwa ya kimkakati inayolenga kuongeza thamani ya madini nchini.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa Serikali kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi hiyo, ikiwemo kuimarisha usimamizi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ukaribu zaidi ili kuhakikisha zinatimiza majukumu yake ipasavyo.
“Kamati inaishauri Wizara kuendelea kuwa makini katika utekelezaji wa miradi na kuhakikisha inaendana na malengo ya kitaifa ya maendeleo ya sekta ya madini,” amesema Lusengekile.
Kamati hiyo imeisisitiza Serikali kuwekeza katika miradi ya kimkakati ya uchenjuaji wa madini kwa kutumia teknolojia za kisasa, hatua itakayosaidia kuongeza thamani ya madini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.
.jpeg)
Post a Comment