WIZARA YA MADINI YAOMBA SH. BILIONI 174.98 KWA MWAKA 2026/2027.


WAZIRI wa Madini,Anthony Mavunde,amewasilisha makadirio ya Mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027,na kuomba Bunge liidhinishe Shilingi Bilioni 174.98 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za wizara hiyo.


Akiwasilisha hotuba ya bajeti April 27,2026,Bungeni Jijini Dodoma,Waziri Mavunde amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 71.51 sawa na asilimia 40.87 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.


Amesema shilingi bilioni 103.47 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida  sawa na asilimia 59.13 ya bajeti yote, ikiwa ni pamoja na kugharamia shughuli za kila siku za uendeshaji wa wizara na taasisi zake.


Waziri Mavunde amesema  kuwa ndani ya fedha za matumizi ya kawaida, shilingi bilioni 27.36 zimetengwa kwa ajili ya mishahara ya watumishi, huku shilingi bilioni 76.11 zikielekezwa kwenye matumizi mengineyo ya kiutendaji.


Amesema utekelezaji wa bajeti hiyo utawezesha kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli unaolengwa kufikia shilingi trilioni 1.4 sambamba na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali madini nchini.

No comments