KATIBU WA HAZINA SPORT CLUB AZIPONGEZA TIMU ZA WIZARA YA FEDHA KWA UMAHIRI MCHEZONI


Katibu wa Hazina Sport Club, Bw. Juma Kimolo, amesema kuwa Timu za Wizara ya Fedha ikiwemo Timu ya Mpira wa Miguu, Pete (Netball) na kuvuta kamba zimefanya vizuri katika michezo inayoendelea Mkoani Njombe kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani Meimosi 2026.


Bw. Kimolo amesema kuwa licha ya kutoshika nafasi za juu katika michezo hiyo, timu zake zilionesha uwezo mkubwa mchezoni jambo lililozifanya kuwa gumzo kwa watazamaji kwa umahiri wake.


Amesema kuwa Makocha wa Timu zote wameona ubora na udhaifu wa timu pinzani, jambo linalowafanya kuja na mbinu mbadala za ushindi kwa mashindano yajayo.


Aidha, Bw. Kimolo amezipongeza timu zote za Hazina kwa juhudi walozoonesha na kuwataka kuongeza uwezo na maarifa ili michezo ijayo waweze kufanya vizuri zaidi ikiwemo kushika nafasi za juu.


Alisema kuwa michezo inaleta furaha, inaimarisha viungo vya mwili na kuongeza umoja na mshikamano wa kitaasisi, Wizara na Taifa kwa ujumla.








No comments