VIPAUMBELE NANE VYA WIZARA YA MAWASILIANO HIVI HAPA.



SERIKALI kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,katika mwaka 2026/2027,imejipanga kuimarisha ulinzi wa anga ya mtandao ili kukabiliana na vitisho vya kidijitali vinavyoendelea kuongezeka.


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki,amesema hayo April 30,2026,Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027,iliyobeba vipaumbele nane.


Pia itatunga na kuhuisha sera na miongozo ya sekta, kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu na posta, pamoja na kuweka mazingira rafiki ya kukuza biashara mtandao.


Aidha, serikali inalenga kuendeleza miundombinu ya TEHAMA na kuhakikisha nchi inanufaika kikamilifu na uchumi wa kidijitali sambamba na kuchochea ubunifu kwa kusaidia kampuni changa (startups) kupata mazingira bora ya kukua.


Amesema  uwekezaji katika TEHAMA na programu za anga za juu pia umepewa kipaumbele, huku elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia na teknolojia zinazoibukia ikipewa uzito wa kipekee.


Katika utekelezaji wa majukumu yake, wizara imepanga kuendeleza sera muhimu ikiwemo Sera ya Anga za Juu ya mwaka 2026 na kukamilisha Sheria ya Anwani za Makazi, hatua itakayorahisisha utambuzi wa maeneo na utoaji wa huduma kwa wananchi.


Waziri Kairuki amesema katika eneo la miundombinu, wizara itasimamia ufanisi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na vituo vya kuhifadhi data, huku ikitekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Brodibendi na Mpango Kabambe wa Miundombinu ya TEHAMA wa mwaka 2026–2036.


Aidha, katika kukuza huduma za kidijitali, serikali imepanga kuanzisha Mpango wa Kitaifa wa Mageuzi ya Kidijitali, kuratibu uanzishwaji wa vituo saba vya ubunifu, na kuwezesha uuzaji wa mifumo ya TEHAMA nje ya nchi





No comments