MMUYA ATATUA MIGOGORO YA ARDHI HADI USIKU
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Kaspar Mmuya ameonesha uongozi wa vitendo kwa kufanya kazi hadi saa mbili usiku kusikiliza na kushughulikia changamoto za sekta ya Ardhi.
Hatua hiyo Ilikuwa ni mwitikio wa utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mwigulu Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyesisitiza viongozi wa sekta ya ardhi kushughulikia kwa kasi migogoro iliyobainika wakati wa ziara yake mkoani Dodoma.
Mhe Mmuya leo Aprili 21, 2026 aliongoza kliniki maalum ya migogoro ya ardhi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliyofanyika Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma ambapo alipokea, kusikiliza na kufuatilia malalamiko ya wananchi yaliyosasilishwa hadi saa mbili usiku
Wakati wa Kliniki hiyo Mhe Mmuya alihakikisha hakuna mwananchi yeyote aliyejitokeza na kubaki bila kusikilizwa huku akisimamia kwa karibu uchambuzi na ufuatiliaji wa kila shauri la mwananchi.
Katika kinachooneka kuimarisha ufanisi Mhe. Mmuya ameagiza wataalamu wa sekta ya ardhi kwenda uwandani kuhakiki na kukusanya taarifa sahihi za migogoro ya Ardhi ili kuipatia ufumbuzi wa haraka na wa kudumu kufikia ijumaa wiki hii.
Hatua hiyo inalenga kuongeza imani ya wananchi kwa Serikali kuimarisha usimamizi wa ardhi na kuharakisha upatikanaji suluhu ya migogoro ya Ardhi iliyodumu kwa muda mrefu
Uamuzi wa mhe. Mmuya kumfanya kazi hadi usiku unatokana na maelekezo yaliyotolewa Aprili 19 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba aliyewataka viongozi na wataalamu wa sekta ya ardhi kushughulikia kwa haraka migogoro iliyobainishwa wakati wa ziara yake mkoani Dodoma.
Katika Kliniki hiyo maaluma kulikuwa na idadi kubwa ya wananchi wenye malalamiko yaliyohusu migogoro ya mipaka, umiliki na matumizi ya ardhi ambapo mhe. Mmuya alisikiliza kila shauri kwa umakini, akihakikisha hakuna mwananchi anayepuuzwa.

.jpeg)









Post a Comment