WAAJIRI WA WAUGUZI WATAKIWA KULIPA STAHIKI ZA WAUGUZI MKOANI MARA



Mkutano Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) Mkoa wa Mara umefanyika leo tarehe 11 Aprili, 2026 katika ukumbi wa Mwembeni Complex .


Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Humphrey Kong'oke amewataka waajiri wa Wauguzi katika Mkoa wa Mara kulipa madai ya stahiki za Wauguzi kwa wakati.

Ndugu Kong'oke pia amewapongeza Wauguzi wote kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuimarisha afya za wananchi wa Mkoa wa Mara na Watanzania kwa ujumla.

Mkoa wa Mara una jumla ya Wauguzi 1, 903 walioajiriwa na Serikali, taasisi binafsi na taasisi za Dini wanaotoa huduma katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya.











No comments