𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄 𝐋𝐀𝐏𝐈𝐓𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐄𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐖𝐈𝐙𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐋𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐓𝐑𝐈𝐋𝐈𝐎𝐍𝐈 1.8 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐊𝐀 2026/27
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Wizara ya Afya ya Shilingi trilioni 1.8 kwa mwaka wa fedha 2026/27, ikiwa ni hatua muhimu katika kuendelea kuimarisha huduma za afya nchini.
Bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Afya, 𝐌𝐡𝐞. 𝐌𝐨𝐡𝐚𝐦𝐦𝐞𝐝 𝐌𝐜𝐡𝐞𝐧𝐠𝐞𝐫𝐰𝐚 (𝐌𝐁), inalenga kuongeza ubora wa huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kuendeleza miundombinu ya hospitali pamoja na kusogeza huduma bora kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Kati ya fedha zilizopitishwa, Shilingi trilioni 1.148 sawa na asilimia 64 zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo huku Shilingi bilioni 652.236 zikitumika kwa matumizi ya kawaida ya wizara hiyo.
Aidha, kupitia bajeti hiyo serikali itaendelea kusimamia maboresho makubwa katika sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, upatikanaji wa wataalamu pamoja na kuimarisha huduma za kibingwa.

Post a Comment