DKT. SAMIA ALIPA TZS. 76 BILIONI ADA YA UANDAAJI MASHINDANO YA AFCON 2027 NCHINI TANZANIA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameridhia na kutoa kiasi cha Dola za Marekani 30,000,000 sawa na shilingi 76,157,100,000 kama ada ya uandaaji wa mashindano ya AFCON2027 yanayotarajiwa kufanyika nchini kuanzia tarehe 19 Juni hadi 17 Julai, 2027.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, leo Bungeni Jijini Dodoma, Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo, Mhe. Paul Makonda (MB) amesema hii ndiyo tafsiri halisi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kama mwanamichezo namba 1 nchini ambaye amedhihirisha dhamira ya dhati ya Serikali katika kufanikisha mashindano ya AFCON2027.

Mhe. Makonda ameridhibitishia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa kuelekea mashindano ya AFCON 2027, Wizara hiyo imejipanga kikamilifu kwa kushirikisha wadau wote kuhakikisha mashindano hayo siyo tu yanafanyika bali yanaweka historia na alama isiyofutika nchini.

No comments