JAMII ZAKATIKIWA KUNEDELEA KUHIMIZA USAWA KIJINSIA ILI KUCHOCHEA MAENDELEO YA PAMOJA
Jamii imehimizwa kuwa na usawa wa kijinsia kwa wanawake katika jamii ili kusukuma gurudumu la maendeleo lengo kuwe na mshikamano katika majukumu ya kila siku kwani imeonekana wanawake hawapewi usawa katika jamii.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Upendo Manase kutoka Taasisi ya Asedeva na ni Mratibu wa Mradi wa Jinsia amesema kuwa mradi huwa unalenga kupandana na ukosefu kwa kijinsia kupitia nguvu ya sanaa kwani wasanii wananguvu kubwa katika jamii .
Aidha, Upendo amesema mradi huo utafanyikia katika Mkoa wa Dar es Salaam Wilaya ya Kinondoni ambapo watafanya manonesho 30 ,manonesho ili kuwawezesha wanawake kumiliki na kusimulia hadidhi zao.
Nao wasanii wanashiriki Katika Mradi wa Jinsia Ke Jafary Bandukini na Irene Lugakingila wamesema hawajaigiza tu katika Mradi huo Bali lengo ni jamii iweze kutambua umuhimu wa usawa wa kijinsia.

Post a Comment