REA NA SHIRIKA LA MIZINGA KUENDELEZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA



Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Mzinga, wamesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano yanayolenga kuimarisha ushirikiano katika Utafiti, Teknolojia, Uzalishaji na Usambazaji wa nishati safi ya kupikia.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga, Balozi Luteni Jenerali (Mstaafu), Charles Makakala, amesema utekelezaji wa mpango huo utakuwa msaada mkubwa kwa wanawake wa vijijini ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kutafuta nishati kwa ajili ya kupikia.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali (Mstaafu), Jacob Kingu, amesema ushirikiano huo utaongeza uzalishaji wa mkaa mbadala utokanao na mabaki ya mimea pamoja na uzalishaji wa majiko banifu kwa bei nafuu zaidi na hivyo kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.


Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amesema makubaliano hayo pia yanakwenda kuongeza aina za nishati safi za kutumika zenye gharama nafuu zaidi lengo likiwa kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia.






No comments