REA YAANDIKA HISTORIA LUDEWA, YAWASHA UMEME
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijni-REA, unaendelea kutekeleza miradi pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa na watakaopewa zabuni ya kutekeleza miradi ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa ili iweze kuwanufaisha wananchi.
Hayo yamebainishwa na Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, wakati wa wakikagua miradi, kutembelea na kuwasha umeme kitongoji cha Nkanda kilichopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe mradi uliokuwa unatekelezwa na Suma Jkt Electric Company Ltd.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Deogratius Nagu amesema katika kitongoji cha Nkanda takribani shilingi milioni-450 zimetolewa na Serikali kupitia REA ili kufikisha huduma ya umeme katika kitongoji hicho.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Suma JKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, ameishukuru REA kwa kuwapatia kazi hiyo ya kufikisha umeme katika maeneo ya mwambao kikiwemo kitongoji hicho cha Nkanda ambapo kazi imekamilika kwa ubora.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameeleza namna ambavyo Mradi huo umekuwa mkombozi kwao.





Post a Comment