TUTAHAKIKISHA CHANGAMOTO ZINATATULIWA ILI KUITUMIA FURSA ILIYOPATIKANA-WAZIRI KAPINGA.



Serikali imesema itahakikisha inashughulikia  changamoto zilizopo kwa wafanyabiashara ili kuitumia fursa ya kuuza bidhaa bila ushuru nchini China.

  Hayo yamebainishwa Leo na Waziri wa Viwanda na biashara Judith Kapinga wakati akizungumza na wadau wa biashara kuhusu fursa ya kuuza bidhaa China bila Ushuru.

   Amesema Wizara yake inaendelea kushirikiana na Wizara nyingine pamoja na taasisi nyingine za Serikali ili kutatua changamoto zilizopo na zitakazojitokeza ili kuitumia Vema fursa hiyo.

  Ameongeza kuwa endapo fursa hiyo ikitumika kikamilifu taifa litapiga hatua kubwa kibiashara na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara Afrika na Duniani kwa ujumla.

  Awali  Balozi wa China hapa nchini  Chen  Mingjian amesema kuwa toka Mei most mwaka huu tayari nchi 33 zimeanza kuuza bidhaa bila ushuru nchini China ( zero interest)






No comments