WANAFUNZI 315,307 WADAHILIWA KATIKA VYUO CHA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI 2025/206
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf F. Mkenda, amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya amali nchini kwa lengo la kuongeza fursa za vijana kupata ujuzi na kujiunga na soko la ajira.
Amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26, jumla ya wanafunzi
315,307 wamedahiliwa katika vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi
stadi, idadi ambayo imezidi lengo la wanafunzi 265,000, sawa na asilimia 119 ya
utekelezaji. Aidha amebainisha kuwa ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa
idadi ya vyuo vya ufundi kutoka 1,414 hadi 1,446 nchini.
Akiwasilisha
makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo Mei 7,2026 bungeni jijini
Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameongeza
kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo 64 vya VETA vya wilaya pamoja na
chuo kimoja cha Mkoa wa Songwe, ambapo ujenzi huo umefikia wastani wa asilimia
68, hatua inayolenga kusogeza huduma za mafunzo ya ufundi karibu zaidi na
wananchi.
Amesema kuwa Serikali kupitia
Wizara imeendelea pia kuboresha miundombinu ya mafunzo ikiwemo ujenzi wa
maabara za TEHAMA katika shule na vyuo vya ufundi ili kuongeza ubora wa
ufundishaji na ujifunzaji.
Aidha amebainisha kuwa Serikali
imeweka mkazo katika kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaohitajika sokoni
kupitia mafunzo ya vitendo, ili kuwawezesha kujiajiri na kuajiriwa katika sekta
mbalimbali za uchumi.
Pia ameongeza kuwa juhudi hizo
ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha elimu ya amali nchini na
kuhakikisha vijana wanakuwa na ujuzi unaokidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda.

Post a Comment