WAZIRI MKENDA AAINISHA VIPAUMBELE WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA VINAVYOZINGATIA UTEKELEZAJI SERA YA ELIMU
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, imeainisha vipaumbele vya bajeti kwa kuzingatia mahitaji ya utekelezaji wa Sera ya Elimu inayolenga kuimarisha ubora wa elimu, kukuza ujuzi na kuongeza maarifa.
Akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma leo Mei 7, 2026, Waziri Adolf Mkenda amesema kutokana na mwelekeo huo Wizara itaendelea kuweka jitihada kubwa katika maandalizi ya elimu ya lazima ya miaka 10, elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, matumizi ya TEHAMA na kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuendana na mahitaji ya Dira 2050.
Aidha, Prefesa Mkenda amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itajielekeza kutekeleza vipaumbele ikiwemo kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria, kuandaa miongozo na kutoa mafunzo nchini, kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa mafunzo ya amali katika shule za sekondari na vyuo vya amali, uongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu, kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuimarisha uwezo wa nchi katika utafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Post a Comment