ZAWADI LIGI YA MUUNGANO KUBORESHWA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Hamad Yussuf Masauni amesema msimu ujao wa Ligi ya Muungano 2026 utaboreshwa zaidi, ikiwemo kuongeza thamani ya zawadi kwa bingwa ili kuipa hadhi na mvuto mkubwa ligi hiyo.


Akizungumza mjini Unguja wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za ligi hiyo, Masauni alisema serikali za Tanzania na Zanzibar zinaendelea kutumia michezo kama nyenzo ya kuimarisha umoja na mshikamano wa Watanzania.


Katika fainali ya ligi hiyo, Simba SC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Young Africans SC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan Complex.


Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Dkt. Riziki Pembe Juma amesema mafanikio ya msimu huu yameongeza hamasa ya kuanza mapema maandalizi ya msimu ujao.








No comments