QWARAY AIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WIKI YA UTUMISHI WA UMMA



NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa juhudi kubwa inayofanya katika kuhudumia wananchi hususani katika  Maadhimisho ya Wiki wa Utumishi wa Umma 2026.


Mhe. Qwaray amesema kuwa  wingi wa wananchi wanaofika katika banda hilo ni ishara tosha kuwa Wizara hiyo imejipanga vyema kutoa huduma bora inayo waridhisha wananchi. 


Pamoja na kutoa pongezi hizo, Naibu Waziri huyo pia amesema ni imani yake kuwa, watumishi wa Wizara hiyo watajipanga vizuri zaidi katika ubunifu wa kuwahudumia watalii watakaomiminika msimu wa Fainali za Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kama sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa inayofanya na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutangaza Utalii nchini. 


Pamoja na Mhe. Qwaray, viongozi wengine waliotembelea  banda hilo lenye mvuto adimu, ni pamoja na  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Mkomi, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Bernard Marcelline,  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania  (TAWIRI),  Dkt. Eblate  Mjingo  na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Emmanuel Buhohela. 


Maadhimisho hayo ya kila mwaka yameanza  Juni 16, 2026 na yatahitimishwa Juni 23, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma.















No comments