SERIKALI, WADAU WATOA HUDUMA ZA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO - TABORA



Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Afya ikiwemo Shirika la Kimataifa la Helen Keller (Helen Keller International) imeweka kambi maalum ya huduma za upasuaji wa kumtoa mtoto wa jicho katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora. 


Mmoja wa mnufaika wa huduma hiyo Bw. Henry Machibya (62) leo Juni 09, 2026 amesema kuwa tatizo lake la macho lilianza mwaka 2023, lakini katika kipindi cha miezi Mitano iliyopita hali ilizidi kuwa mbaya na kupelekea kupoteza uwezo wa kuona kabisa kwa macho yote mawili hadi kushindwa kuendelea na shughuli zake za kilimo ambazo zilikuwa chanzo chake kikuu cha mapato.


"Nilikuwa nikitegemea kilimo kwa ajili ya kujikimu na kuhudumia familia yangu, lakini hali ya macho yangu ilibadilisha maisha yangu kabisa," hayo ni maneno ya Mzee Henry Damas Machibya mkazi wa Simbo wilayani Igunga Mkoani Tabora ambaye hujishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara.


Aidha, Mzee Machibya amesema kwa sasa anapitia changamoto kubwa ikiwemo kusindikizwa chooni, kushindwa kufanya shughuli zake za msingi za kila siku ikiwemo kilimo, kutambua chakula anachokula huku akitegemea msaada wa watu wa karibu katika maisha yake ya kila siku.


Kupitia kambi ya uchunguzi na matibabu ya mtoto wa jicho inayofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mzee Machibya amepata fursa ya kupata huduma za kibingwa bila gharama zilizodhaminiwa na Wadau wa Sekta ya Afya nchini. 


Wananchi wote wenye changamoto za uoni wanahimizwa kujitokeza mapema kwa uchunguzi na matibabu katika kambi hiyo bila malipo ambayo imefanikishwa kupitia ushirikiano kati ya OWM-TAMISEMI, Wizara ya Afya na Shirika la 'Helen Keller International' kwa lengo la kurejesha nuru na matumaini ya maisha kwa Watanzania takbiban  700( Mia Sana) wa Mkoa wa Tabora














No comments