DKT KIJAJI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 48 WA KAMATI YA URITHI WA DUNIA
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji leo Julai 23, 2026 ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 48 wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendelea Mjini Busan Jamhuri ya Korea
Katika mkutano huo pia Waziri Kijaji amepata wasaa wa kukutana na kufanya mazungumzo na Kamati ya ushauri masuala ya Uhifadhi wa Maeneo ya Urithi wa Asili ya shirika la elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa 'UNESCO' ambapo ameeleza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania katika kuimarisha uhifadhi katika maeneo ya urithi wa dunia ikiwemo Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.













Post a Comment