MPANGO WA DHARURA WA TAIFA WA KUKABILIANA NA MADHARA YA EL NIÑO WAIDHINISHWA



Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu ya Usimamizi wa Maafa imeidhinisha Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El Niño na kuzielekeza Wizara, Idara, Taasisi, Mikoa na Halmashauri kuongeza kasi ya maandalizi ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño zinazotabiriwa kudumu hadi mwisho wa mwaka 2026.


Akizungumza Jijini Dar es salaam  katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, ameelekeza kila sekta kutenga rasilimali zitakazowezesha hatua za kuzuia, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali katika eneo lake na pia kuandaa mipango ya dharura ya manunuzi.


Amesisitiza umuhimu wa kutambua mapema maeneo hatarishi, kufanya tathmini za vihatarishi, kuwahamasisha wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kuhamia maeneo salama na kuandaa mipango ya kuzuia milipuko ya magonjwa kwa binadamu, mifugo na mimea.


Aidha,ameagiza ukaguzi na uboreshaji wa miundombinu muhimu ikiwemo barabara, maji na umeme, kuimarisha usimamizi wa mazingira, kuhakikisha vifaa vya uokoaji, huduma za dharura na mifumo ya mawasiliano vinakuwa tayari wakati wote, pamoja na kuhuisha mipango ya utekelezaji katika maeneo hatarishi








No comments