MASAUNI: MUUNGANO NI TUNU YA TAIFA ISIYOPASWA KUCHEZEWA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, amesisitiza umuhimu wa kuuenzi na kuuheshimu Muungano wa Tanzania, akieleza kuwa ni tunu ya taifa isiyopaswa kuchezewa.
Masauni ameeleza, Muungano ndio msingi wa umoja na maendeleo ya Taifa, hivyo Watanzania wanapaswa kuuenzi na kujivunia mafanikio yaliyopatikana kupitia ushirikiano huo.
Akizungumza Chalinze, wilayani Bagamoyo, wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Pwani, Julai 22,2026 Masauni amepongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayochochea shughuli za kiuchumi kati ya Bagamoyo na Zanzibar.
Aidha, Masauni amewaasa vijana kupuuza baadhi ya taarifa zinazopotosha kuhusu masuala mbalimbali yaliyoasisiwa na waasisi wetu, huku akiwahimiza kutumia mitandao ya kijamii kwa tija.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Ridhiwani Kikwete, ameeleza greda hilo, litasaidia kuokoa muda na gharama zilizokuwa zikitumika kuboresha miundombinu ya barabara za ndani, hivyo fedha hizo sasa zitaelekezwa katika utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga, ameishukuru Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuufungua mji wa Bagamoyo kiuchumi, akieleza kuwa zaidi ya Sh bilioni 27 zilitolewa mwaka uliopita kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amefafanua
Kunenge ameongeza kuwa ili Mkoa wa Pwani uendelee kunufaika na mageuzi ya kiuchumi, kuna haja ya kuhamasisha uwekezaji wa hoteli kubwa na za kisasa zitakazovutia wawekezaji na watalii wengi zaidi.
Mkuu huyo wa Mkoa amemuomba Waziri Masauni kufikisha ombi la Halmashauri ya Chalinze kuwa Manispaa kutokana na kuwa na vigezo vingi kikiwemo cha ongezeko la kukua kwa mapato.









Post a Comment