KAMATI YA USHAURI WA AFYA YA KITAALAM UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI YAKUTANA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, leo Agosti 17, 2026 jijini Dar es Salaam ameongoza Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Ushauri ya Afya ya Kitaalam ya Ukanda wa Afrika Mashariki (ReTAC), unaolenga kujadili na kuweka mikakati ya kuimarisha usalama na kujitegemea kwa afya barani Afrika.
Mkutano huo pia umejikita katika kuandaa mapendekezo kuhusu uwekezaji endelevu unaotabirika na bunifu katika afya ya mama na mtoto pamoja na huduma za afya ya msingi kuelekea Mkutano wa Mawaziri wa Afya wa Afrika Mashariki unaofanyika kesho Agosti 18, 2026 jijini Dar es Salaam.

Post a Comment