TOSCI YAONYA DHIDI YA MBEGU BANDIA



Wakulima wa mahindi nchini wametakiwa kuhakiki ubora wa mbegu kabla ya kupanda ili kujikinga na mbegu bandia na zisizokidhi viwango ambazo zinaweza kusababisha hasara na kupunguza mavuno.


Wito huo umetolewa jijini Mwanza na Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya mbegu zilizothibitishwa.


Kwa mujibu wa takwimu za TOSCI, mahindi yalichangia asilimia 93 ya mbegu zote zilizothibitishwa nchini katika mwaka wa kilimo 2025/26, hata hivyo, mfumo rasmi wa mbegu unachangia takribani asilimia 40 pekee ya mbegu zinazotumika nchini, huku asilimia 45 zikitoka kwenye mfumo usio rasmi.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bayer Life Science Tanzania, Mwinyi Sango, amesema mabadiliko ya tabianchi yameongeza umuhimu wa wakulima kutumia mbegu bora zinazofaa mazingira husika ili kuongeza uzalishaji na kupunguza athari za misimu isiyotabirika.



No comments