NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA) DKT. MADUHU KAZI AZURU NEMC



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Maduhu Kazi, amezuru NEMC kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  kushika wadhifa huo.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Kazi ameipongeza Serikali kwa kuthamini masuala ya Mazingira na kuipa kipaumbele ajenda ya mazingira katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, akisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha maendeleo ya Taifa yanaenda sambamba na uhifadhi endelevu wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.


Aidha, ameipongeza NEMC kwa uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yake na kulitaka Baraza kuendelea kusimamia misingi ya Sheria, huku likiimarisha ufanisi katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa manufaa ya Taifa na vizazi vya baadae.


Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi alipokuwa akizungumza alimweleza Dkt. Kazi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza na hatua zinazochukuliwa katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira, huku akiahidi kuendelea kusukuma mbele ajenda ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa kuzingatia Sheria, Kanuni  na miongozo ya Serikali.











 *

No comments