TEN/MET YAANDAA WARSHA YA WAANDISHI KUHUSU TAALUMA YA UALIMU
Mtandao wa Elimu Tanzania TEN/MET umeandaa warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari na wahariri, inayolenga kuangazia taaluma ya ualimu na namna vyombo vya habari vinavyoripoti na kuiwasilisha kwa umma.
Warsha hiyo inafanyika jijini Dar es Salaam, ikiwakutanisha waandishi na wahariri kwa lengo la kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kuibua na kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu taaluma ya ualimu.
Kupitia warsha hiyo, washiriki wanajadili namna ya kuboresha uandishi wa habari kuhusu elimu, ikiwemo kuzingatia usahihi wa taarifa, uwiano wa habari na uwasilishaji unaosaidia jamii kuelewa changamoto na fursa zinazowakabili walimu.
TEN/MET inaendelea kusisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kuhakikisha masuala ya elimu na taaluma ya ualimu yanapewa nafasi na kuwasilishwa kwa umma kwa mtazamo unaojenga.
Warsha hiyo pia inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa elimu na wanahabari katika kuibua mijadala yenye tija kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment