ORCI KUANZA UPASUAJI MKUBWA WA SARATANI OKTOBA
Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) inatarajia kuanza kutoa huduma za upasuaji mkubwa wa saratani mwezi Oktoba mwaka huu, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa vyumba vya upasuaji.
Hatua hiyo ni sehemu ya uwekezaji unaolenga kuimarisha huduma za matibabu ya saratani nchini na kuiwezesha ORCI kutoa huduma zote za matibabu ya kibingwa ya saratani katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 19,2026,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt.Diwani Msemo amesema madaktari bingwa saba wa upasuaji tayari wamesharejea kutoka masomoni, wakiwa wamebobea katika maeneo ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya wanawake na upasuaji wa ujumla, huku wataalamu wengine wanne wakiendelea na masomo.
Amesema kuanza kwa huduma hiyo kutaimarisha uwezo wa Taasisi katika kutoa huduma za matibabu ya saratani, sambamba na kuendelea kuboresha huduma za kibingwa na kibingwa bobezi kwa wagonjwa.
Hatua hiyo inaenda sambamba na miradi mingine inayotekelezwa na ORCI katika kuboresha miundombinu, vifaa tiba, huduma za uchunguzi na tiba ya mionzi kwa lengo la kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora, salama na kwa wakati.
.jpeg)
Post a Comment