TANZANIA YAZINDUA JUKWAA LA NANE LA WADAU WA MAENDELEO YA BONDE LA MTO NILE



Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amefanya uzinduzi huo jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Maji.


Lengo la jukwaa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa nchi  washirika wa Bonde la Mto Nile katika kutafuta suluhisho bunifu za kugharamia miundombinu ya maji na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.


Mhandisi Mwajuma amesema Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa jukwaa  akisisitiza kuwa Tanzania ni mshirika muhimu katika bonde hilo hasa kutokana na ukweli kuwa Mto Nile chanzo chake kikubwa ni  ziwa Victoria ambalo sehemu yake ipo Tanzania


Ameeleza kuwa Bonde la Mto Nile linakabiliwa na changamoto zinazoongezeka kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la idadi ya watu na matumizi, ukuaji wa uchumi pamoja na mahitaji makubwa ya maji, chakula na nishati. 


Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Bonde la Nile  Mhandisi Nestor Niyonzima ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushiriki katika kuwasilisha maandiko na habari mbalimbali ambazo zinazohusu   Bonde la Mto Nile kwa lugha mbalimbali, ikiwamo Kiswahili.






No comments