WAZIRI MCHENGERWA AONGOZA MKUTANO WA NNE WA KAMATI YA UONGOZI YA MAWAZIRI WA AFYA WA UKANDA WA AFRIKA (RESCO)
Waziri wa Afya, 𝐌𝐡𝐞. 𝐌𝐨𝐡𝐚𝐦𝐦𝐞𝐝 𝐌𝐜𝐡𝐞𝐧𝐠𝐞𝐫𝐰𝐚 (𝐌𝐁), akiongoza Mkutano wa Nne wa Kamati ya Uongozi ya Mawaziri wa Afya wa Ukanda wa Afrika (ReSCO), unaofanyika leo Agosti 19, 2026, jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo, ulioanza jana Agosti 18, 2026, unawaleta pamoja Mawaziri kutoka nchi 14 za Ukanda wa Afrika kujadili na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama, mtoto na vijana, pamoja na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na kuimarisha mifumo ya afya katika ukanda huo.
Mhe. Mchengerwa ni Mwenyekiti wa Mkutano huo, unaowakutanisha Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali za Ukanda wa Afrika kwa lengo la kujadili changamoto za afya na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana nazo.
Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Elias Mgembe, anashiriki katika mkutano huo pamoja na viongozi na wataalamu wengine wa afya. Washiriki wanajadili masuala ya msingi yanayolenga kuimarisha mifumo ya afya na usalama wa afya katika Ukanda wa Afrika.












Post a Comment