DKT. MWINYI: MAFUNZO YA MAKADA WAKUFUNZI NI MUHIMU KATIKA KUKIIMARISHA CCM



Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema mafunzo ya makada wakufunzi ni muhimu katika kuimarisha Chama kuanzia ngazi za chini, kwa kuhakikisha misingi, itikadi, historia na maadili ya CCM vinaeleweka na kufikishwa kwa wanachama kwa usahihi.


Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 30 Septemba 2026, wakati akifunga Mafunzo ya Wakufunzi wa Makada wa CCM Awamu ya Pili yaliyofanyika Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.


Amesema jumla ya makada 840 wamepatiwa mafunzo kupitia programu hiyo, huku akiwataka wakufunzi hao kuimarisha elimu ya Chama, matumizi ya teknolojia ya kidijitali, pamoja na kuimarisha mashina na matawi katika kusikiliza na kushughulikia kero za wanachama na wananchi.





















No comments