MAAFISA WANAWAKE MAGEREZA 'WAPIGWA MSASA' SHULE YA UONGOZI
Mafunzo hayo ya muda mfupi yalianza tarehe 21 Septemba 2026 hadi tarehe 25 Septemba 2026 yakihusisha kozi ya Uongozi na Usimamizi Endelevu na Jumuhishi kwa wanawake (Sustainable and Inclusive Women Leadership and Management - SIWOLEMA)
Wanawake viongozi wa Jeshi la Magereza walioteuliwa kuhudhurua mafunzo hayo ni; ACP. Matrida Mlawa - Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, ACP. Mwanaamina Msangi - Utawala Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, SSP. Nimwindael Mziray - Mkuu wa Gereza Wanawake Kingolwira, SSP. Bonanza Malata - Mhandisi Makao Makuu ya Jeshi, SSP. Amina Lidenge - Mhasibu Makao Makuu ya Jeshi, SSP. Tekla Ngilangwa - Mkuu wa Gereza Kongwa, SSP. Rehema Okelo - Mkuu wa Kiwanda cha viatu Kilimanjaro na SSP. Hamida Matimba - Mkuu wa Sehemu ya wanawake Gereza Segerea.
Mafunzo hayo ya viongozi 59 wakiwemo wa Jeshi la Magereza, yalihusisha taasisi nyingine za TTCL TCRA, PPRA, NSSF, IRUWASA, NDC, Bodi ya Korosho, Bodi ya Chai, na nyinginezo.
Aidha baada ya kukamilika mafunzo hayo, wahitimu wanawake viongozi wa Jeshi la Magereza walipata fursa ya kukutana na Mkuu wa Jeshi katika ofisi ndogo iliyoko Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 28 Septemba 2026 lengo likiwa ni kutoa mrejesho wa Mafunzo hayo.

Post a Comment