DUDU BAYA ALIPIWA FAINI YA MILIONI TATU NA WAANDAAJI WA TAMASHA LA MIAKA 30 YA BONGO FLEVA
Waandaaji wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva, wameutangazia Umma kuwa tayari wamelipa faini ya Shilingi Milioni tatu waliyopigwa na BASATA, kama waandaaji na kumlipia msanii waliye mpandisha katika tamasha lao Ndg. Godfrey Tumaini (Dudubaya), baada ya kukiuka Sheria za nchi.
Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa mmoja wa waandaaji wa Tamasha hilo, Ndg. Hamad Seneda (Madee) ameandika, "Baada ya kupokea maamuzi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), tunapenda kuujulisha umma kuwa tumepokea na kukubali kutekeleza adhabu zilizotolewa na Baraza hilo na kwaharaka Tumeshalipa FAINI
Katika kutekeleza maamuzi hayo, tumelipa FAINI iliyotolewa kwa waandaaji, pamoja na kulipia FAINI iliyotolewa kwa msanii Godfrey Tumaini, maarufu kama Dudubaya.
Tunapenda kuihakikishia BASATA na wadau wote wa sanaa nchini kuwa tunaheshimu maamuzi hayo na tumejipanga kutekeleza wajibu wetu kwa kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa.
Tunaamini kuwa ushirikiano, uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria ni misingi muhimu katika kulinda, kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa nchini.
Tunatoa shukrani kwa BASATA na wadau wote kwa ushirikiano wao, huku tukiahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka husika katika kuhakikisha sekta ya sanaa inakua na kuendelezwa kwa kuzingatia misingi ya kisheria na kitaaluma."

Post a Comment