MARY NCHIMBI AFARIKI DUNIA


Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Jumuiya ya Vijana, Chama pamoja na Ofisi Ndogo ya Lumumba, na kutumikia CCM Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, Mary Nchimbi, amefariki dunia Septemba 13, 2026.


Taarifa za awali zinaeleza Msiba huo unaendelea Boko Temboni, karibu na Kituo cha Watoto Yatima, Kibaha Mjini, huku mwili wa marehemu ukitarajiwa kusafirishwa Jumanne, Septemba 15, kuelekea mkoani Ruvuma kwa ajili ya maziko.


Wakielezea walivyomfahamu  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao, amesema Nchimbi alikuwa mwanasiasa wa muda mrefu na mwalimu, aliyewahi kutumikia chama katika majukumu mbalimbali ya kiutendaji.


Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani, Zainab Vullu, amesema alimfahamu Nchimbi tangu miaka ya 1980, akimtaja kuwa kada mchapakazi, aliyejitolea katika shughuli za chama, mwenye uwezo wa kuunganisha watu na asiye na majivuno.


Naye Katibu Mstaafu wa CCM Mkoa wa Pwani, Sauda Mpambalyoto, amesema wamepoteza mwenzao aliyekuwa mcheshi na mchapakazi, huku Diwani wa Viti Maalum Kibaha Mjini, Selina Wilson, akisema chama na familia vimepoteza mwanachama na mwanafamilia aliyekuwa kiungo muhimu.

No comments