MWANRI AONA MWANGA KATIKA MAZUNGUMZO YA MARIDHIANO YA KISIASA
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Aggrey Mwanri, amesema mazungumzo yanayoendelea kufanyika kati ya wadau mbalimbali kuhusu hali ya kisiasa nchini yameonyesha mwanga mkubwa katika mchakato wa maridhiano na kutafuta mwafaka.
Mwanri ameyasema hayo leo, Septemba 7, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini, uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Amesema mjadala uliofanyika umeonyesha utayari wa wadau kusikilizana, kujadiliana na kuweka mbele maslahi ya taifa katika kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali za kisiasa.
Akizungumza kuhusu matarajio yake kabla ya kuwasili kwenye mkutano huo, Mwanri amesema awali alikuwa na wasiwasi kwamba mjadala huo ungeelekezwa zaidi katika kukikosoa chama tawala, CCM, lakini hali iliyojitokeza ndani ya mkutano imekuwa tofauti na matarajio yake.
“Wakati nakuja nilikuwa na kahofu kidogo, nikafikiria kwamba watarusha mawe CCM bana, chama tawala bana, hii shida yote tunayopata ni CCM bana. Tulikuwa na Mzee Wasira, nikamwambia kama mood yenyewe ni hii unaweza kuwa na uhakika kuwa tuko tayari,” amesema Mwanri.
Amesema hali ya majadiliano iliyojitokeza katika mkutano huo ni ishara nzuri kwamba wadau wa kisiasa na makundi mbalimbali nchini wana nafasi ya kufikia maridhiano na mwafaka, kwa kuweka pembeni tofauti zao na kuzingatia maslahi mapana ya Tanzania.
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


Post a Comment