MWENYEKITI WA BARAZA LA VIJANA TAIFA ZANZIBAR, DKT. MOHAMMED ABRAHMAN JUMA, AMEWATAKA VIJANA KUENDELEA KUWA WAZALENDO
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa Zanzibar, Dkt. Mohammed Abrahman Juma, amewataka vijana kuendelea kuwa wazalendo na kulitumikia taifa kwa uaminifu, ili kuhakikisha Zanzibar na Tanzania kwa ujumla inaendelea kuwa na viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza na kuleta maendeleo kwa wananchi.
Dkt. Mohammed ameyasema hayo leo, Septemba 8, 2026, wakati akifungua mafunzo ya uongozi bora kwa vijana wa Mabaraza ya Vijana Zanzibar, yaliyofanyika katika Ukumbi wa ZSSF, Kariakoo, Zanzibar.
Amesema viongozi wanapaswa kuhakikisha wanawajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao na kutimiza kwa ufanisi shughuli zinazohusiana na nafasi walizokabidhiwa na kuaminiwa na wananchi.
Ameeleza kuwa uongozi ni dhamana inayohitaji uwajibikaji, uadilifu na kujituma, hivyo vijana wanaotayarishwa kuwa viongozi wanapaswa kujenga misingi ya uongozi bora tangu sasa kwa kuzingatia maadili, nidhamu na uzalendo.


.jpeg)

.jpeg)


Post a Comment