RAIS DKT. MWINYI: ZANZIBAR YAFUNGUA FURSA MPYA ZA USHIRIKIANO NA URUSI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar iko tayari kuimarisha ushirikiano na Shirikisho la Urusi katika sekta mbalimbali za maendeleo, ikiwemo nishati, bandari na usafirishaji, utalii, elimu na utafiti, afya na Uchumi wa Buluu.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 28 Septemba 2026, alipokutana na ujumbe kutoka Shirikisho la Urusi ulioongozwa na Bw. Denis Agafonov, Mkuu wa Kurugenzi ya Wataalamu katika Ofisi ya Rais wa Shirikisho la Urusi na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar.
Amesema Zanzibar inalenga kutumia fursa za ushirikiano na Urusi katika uwekezaji, teknolojia, utalii, nishati, uvuvi, tafiti za pamoja na maendeleo ya Uchumi wa Buluu, huku akisisitiza umuhimu wa kugeuza maeneo yaliyojadiliwa kuwa miradi yenye matokeo yanayoonekana.
Naye Bw. Denis Agafonov amesema Urusi iko tayari kuendelea kujadiliana na Zanzibar kuhusu maeneo yenye fursa za ushirikiano na uwekezaji.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)


Post a Comment